MAKUNDI YA WANAWAKE WAMTAKA KAREN NYAMU KUJIUZULU

Makundi  ya wanawake yakiongozwa na aliyekuwa seneta maalum Gloria Owuoba sasa yanamtaka seneta Karen Nyamu kujiuzulu kutokana na matamshi yake yaliyomdhalilisha  mwanafunzi wa gredi ya 10 aliyekuwa amezuru bunge la seneti kwa shugli ya masomo. Wanawake hao wanasema Karen Nyamu amekosa heshima kwa wanawake. Imetayarishwa na Hilda Ajema

RAIS RUTO AELEZA UMUHIMU WA CBE NCHINI

Rais William Ruto ameelezea kujitolea kwa serikali katika kuimarisha miundimisingi kwenye taasisi ya elimu ili kupiga jeki shughli  za masomo. Akizungumza wakati wa kongamano la Africa Forward summit  Ruto ameeleza kuwa mfumo wa sasa wa masomo CBE unalenga kuhakikisha wanafunzi wanapata ujuzi wa kutoshawanapotafuta ajira. Imetayarishwa na Hilda Ajema

MIKATABA 11 YA KENYA-UFARANSA KUIMARISHA RELI, BANDARI NA UCHUMI DIJITALI  

Rais William Ruto na mwenzake wa ufaransa Emmanuel Macron wameshuhudia kutiwa saini kwa mikataba 11 inayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Kenya na Ufaransa katika uchukuzi, nishati, miundombinu ya kidijitali na biashara. Mikataba hiyo imetiwa saini katika Ikulu ya Nairobi kufuatia mazungumzo baina ya nchi hizo mbili kabla ya Mkutano wa Africa Forward Summit.Miongoni mwa mikataba muhimu ni ukarabati […]

RASHFORD AWAPA BARCA UBINGWA LA LIGA

Bao la ikabu la Marcus Rashford liliwawezesha Barcelona kuwalaza mahasimu wao Real Madrid kwa kichapo cha mabao 2-0 katika mechi ya La Liga na kutawazwa mabingwa zikiwa zimesalia mechi 3 kabla ya ligi hiyo kutamatika. Mshambulizi huyo wa Uingereza aliwaweka Barcelona kifua mbele kabla ya Ferran Torres kufunga la pili kuwapa miamba hao ushindi katika […]

GOR WALAZIMISHA SARE, LEOPARDS WAPIGWA JEKI

Timu ya Gor Mahia ilipigwa breki katika safari ya kunyakuwa ubingwa wa 22 wa ligi kuu ya soka, KPL, kufuatia sare ya bao 1-1 dhidi ya bingwa mtetezi, Police FC, na kuwapa matumaini AFC Leopards wanaoemezea mate taji hilo. Leopards walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mara Sugar, na sare ya Gor ikipunguza mwanya […]

FKF-WPL: BULLETS WAFYATUA TAJI, TENA

klabu ya Kenya Police Bullets ilijinyakulia taji la tatu la ligi kuu ya soka ya wanawake nchini, FKF-WPL kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Trinity Starlets hapo jana. Kutokana na ubingwa huo, Bullets imekuwa klabu ya kwanza nchini kunyakua ubingwa mara 3 mfululizo katika misimu yake mitatu ya kwanza. Bullets waliingia katika pambano hilo […]

KCB RFC WAELEKEZA DIRA 7S CIRCUIT BAADA YA KURAMBISHWA SUKARI

Kocha mkuu wa klabu ya raga KCB RFC Andrew Amonde, amewahimiza vijana wake kuzika masaibu ya kupoteza kwenye fainali za Kenya Cup siku ya Jumamosi na badala yake kuganga kutetea taji la National Sevens Circuit. KCB ilijinyakulia taji hilo kufuatia ushindi wa 15-14 dhidi ya Strathmore wakati wa fainali ya 2025 Dala Sevens. Hata hivyo, […]

MUSYOKA: KENYA INAVUNA UGOMVI WA FRANCOPHONE

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amepuzilia mbali dhana kwamba Kenya ni kitovu cha kibiashara barani Afrika kutokana na kuteuliwa kwa taifa hilo kuwa mwenyeji wa kongamano la Africa Forward Summit, akisema Kenya inajinufaisha na misukosuko inayoyakabili mataifa ya bara Afrika ambayo huzungumza lugha ya Kifaransa maarufu kama Francophone. Kalonzo amemtaka Rais William Ruto […]

MIKATABA: SEKTA YA RELI KENYA KUVUNA

Ushirikiano wa kidiplomasia na biashara kati ya Kenya na Ufaransa unatarajiwa kuimarika kutokana na mikataba 11 iliyotiwa saini hapo jana na Rais William Ruto na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Ikulu ya Nairobi. Miongoni mwa mikataba hiyo ni ukarabati na uboreshaji wa miundombinu ya reli kwa kima cha shilingi bilioni 12.5, utakaoshuhudia kupanuliwa kwa […]

KINDIKI ATETA KUHUSU USHAHIDI MPYA

Naibu Rais Kithure Kindiki, ameitaka mahakama kuu ya Milimani kuruhusu mawakili kumhoji Daktari wa masuala ya moyo, Dan Gikonyo, kuhusiana na ushahidi wake mpya ulioidhinishwa na mahakama hiyo katika kesi ya kubanduliwa kutoka afisini kwa aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua. Hatua ya Kindiki inajiri siku 3 tu baada ya mahakama hiyo kuidhinisha kutumiwa kwa ushahidi […]