ASILIMIA 25 YA USHURU WA SIMU KUTOATHIRI BEI YA SIMU

Waziri wa Hazina ya kitaifa John Mbadi amepuzilia hofu kwamba Mswada wa Fedha unaopendekezwa wa 2026 utasababisha kupanda kwa bei ya simu mahiri, akisema badala yake kwamba mfumo wa ushuru uliorekebishwa umeundwa ili kupunguza mzigo wa jumla wa ushuru kwenye vifaa vya rununu. Haya yanajiri huku kukiwa na ukosoaji mkubwa wa umma juu ya mapendekezo ya hatua za […]

DEMBELE MCHEZAJI BORA UFARANSA

Mshambulizi wa Paris Saint-Germain Ousmane Dembele hapo jana alitajwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya soka nchini Ufaransa, Ligue 1, ikiwa ni mara ya pili mfululizo baada ya kuwaongoza mabingwa hao wa bara Ulaya kunyakua Ligue 1 na kutinga fainali ya kombe la klabu bingwa bara Ulaya. Dembele mwenye umri wa miaka 28, ni […]

SPURS WASALIA MATATANI NA SARE YA LEEDS

Mathys Tel aliwapandisha Tottenham na kuwazika tena katika eneo la kushushwa daraja baada ya kuwafungia bao na kisha kusababisha penalti iliyowaacha na sare ya bao 1-1 dhidi ya Leeds jana usiku. Matokeo hayo yaliwaacha Spurs katika nafasi ya 17, pointi 2 juu ya West Ham walio katika nafasi ya 18 na kuacha hai kinyang’anyiro cha […]

AKONNOR AWATAKA WACHEZAJI KUMAKINIKA HISTORIA IKIBISHA

Klabu ya Gor Mahia itahitaji ushindi mara 3 pekee katika mechi zake 3 zilizosalia ili kutawazwa mabingwa mara ya 22 katika ligi kuu ya soka nchini, KPL, wakiwa mbele ya wapinzani wao AFC Leopards na pointi 7. Safari ya kuelekea ubingwa huo ilitiwa miiba na sare ya bao 1-1 dhidi ya Police FC wikendi, Gor […]

GHARAMA YA MITUMBA KUPANDA

Huenda Wakenya wanaotegemea biashara za nguo za mitumba wakalazimika kugharamika zaidi kuagiza nguo hizo kutokana na mpango wa serikali kurejesha ushuru wa bidhaa hizo kwenye mwaka wa kifedha wa 2026-27. Kwenye mapendekezo katika mswada wa mwaka ujao wa kifedha, Waziri wa fedha John Mbadi amefafanua kuwa ushuru huo utafanyiwa marekebisho kabla ya kurejeshwa, akihoji kuwa […]

SERIKALI KUWASAIDIA WAATHIRIWA WA MGODI

Familia za walioathirika kutokana na kuporomoka kwa mgodi wa dhahabu katika kaunti ya West Pokot Ijumaa iliyopita, zitapokea msaada wa kifedha kutoka kwa serikali kugharamia matibabu na mazishi kwa watu 15 walioangamia. Haya ni kulingana na Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, akizungumza baada ya kuzitembelea familia hizo katika eneo la Romus, akionyesha masikitiko […]

AFRICA FORWARD SUMMIT KUKAMILIKA LEO

Kongamano la Africa Forward Summit lililoandaliwa kwa pamoja kati ya Kenya na Ufaransa linakamilika hii leo baada ya kuanza rasmi hapo jana jijini Nairobi. Kwenye majadiliano katika kongamano hilo la siku mbili, Rais William Ruto na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron, wameeleza haja ya bara Ulaya kuwekeza katika bara la Afrika, ambalo wamelitaja kama linalokua […]

IEBC YACHACHISHA MAANDALIZI YA CHAGUZI NDOGO

Maandalizi ya chaguzi ndogo katika eneo bunge la Emurua Dikiir na uwakilishi wadi katika wadi mbili za kaunti ya Elgeyo Marakwet na Samburu yameshika kasi huku zikisalia siku mbili kabla ya chaguzi hizo kuandaliwa. Tayari tume huru ya uhaguzi na mipaka, IEBC, imepokea masanduku yenye karatasi za kupigia kura, kabla ya chaguzi hizo za Alhamisi […]

MUSEVENI KUAPISHWA LEO KUENDELEA KUHUDUMU

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ameratibiwa kuapishwa hii leo kuanza muhula wa saba madarakani, baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa hivi punde mapema mwaka huu. Viongozi wa mataifa mbali mbali ya Afrika na kimataifa wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo, akiwemo Rais William Ruto, Samia Hassan wa Tanzania, Felix Tshisekedi wa DRC, Salva Kiir wa […]

AYUB SAVULA AMSUTA GACHAGUA

Naibu Gavana wa kaunti ya  kakamega Ayub Savula amemuonya kiongozi wa chama cha DCP  Rigadhi Gachagua dhidi ya kumshambulia katibu mkuu wa  COTU Francis Atwoli. Savula anasema kuwa matamshi ya Rigadhi dhidi ya Atwoli yanamkosea heshima kiongozi huyo ambaye anashikilia nafasi ya viongozi maarufu katoka jamii ya mulembe. Imetayarishwa na Hilda Ajema