DE ZERBI: HATUJALI KUSHINDA DHIDI YA VILLA ILIYODHOOFIKA

Kocha wa Tottenham Hotspur Roberto De Zerbi amesema hana tatizo lolote na ushindi walioupata dhidi ya Aston Villa licha ya kikosi cha wapinzani hao kuwa na mabadiliko makubwa. Tottenham walishinda mabao 2–1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza, huku Villa wakifanya mabadiliko ya wachezaji wao muhimu ili kujiandaa na mechi za michuano ya Ulaya. […]

WAKENYA WAPEWA NAFASI KUBWA MARATHON YA COPENHAGEN

Wanariadha wa Kenya wanatarajiwa kuwa miongoni mwa washindani wakuu katika toleo la 46 la Copenhagen Marathon litakalofanyika Jumapili nchini Denmark. Vincent Mutai anaongoza orodha ya wanariadha wa wanaume baada ya kumaliza wa pili mwaka uliopita, ambapo aliweka rekodi yake bora ya saa 2:09:09 katika mbio hizo za mji wa Copenhagen. Mutai ni sehemu ya kikosi […]

KCB YAPANIA KUKOMESHA UTAWALA WA KABRAS KENYA CUP

KCB RFC wanaamini wana uwezo wa kukomesha ubabe wa Kabras RFC watakapokutana katika fainali ya Kenya Cup msimu wa 2025/2026 katika uwanja wa ASK mjini Kakamega. Hii itakuwa mara ya nane kwa timu hizo kukutana katika fainali tangu msimu wa 2014/2015, huku Kabras wakisaka taji lao la tano mfululizo katika mashindano hayo. KCB wameingia fainali […]

MUTULA AMKOSOA DUALE KUHUSU KAULI ZA NGAMIA

Gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Jr amemkosoa Waziri wa Afya Aden Duale kufuatia matamshi yake kuhusu ngamia wanaotoka Garissa kuharibu mimea katika maeneo ya Ukambani. Mutula amesema kauli hizo hazifai kutolewa na kiongozi wa kitaifa, hasa wakati ambapo kuna mvutano wa kiusalama katika eneo la Mwingi kati ya wafugaji wa ngamia na wakulima. Amesisitiza kuwa […]

LUSAKA AWAHIMIZA VIJANA KUTUMIA MITANDAO KWA MAENDELEO

Vijana katika Kaunti ya Bungoma  wamehimizwa kutumia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali kama njia ya kujipatia kipato na kujiendeleza kiuchumi. Akizungumza katika eneo la Ndengelwa, Gavana Ken Lusaka amewataka vijana kuacha matumizi mabaya ya mitandao na badala yake kuitumia kwa manufaa yao binafsi. Lusaka ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo […]

KARUA AKOSOA KAULI ZA KAREN NYAMU KWA MWANAFUNZI

Shinikizo linaendelea kuongezeka dhidi ya Seneta mteule Karen Nyamu kufuatia matamshi yake yenye utata dhidi ya mwanafunzi wa Gredi ya Kumi wakati wa kikao cha Seneti. Kiongozi wa People’s Liberation Party Martha Karua ameyataja matamshi hayo kuwa ya kusikitisha na yasiyokubalika, huku akiungana na viongozi wengine wanaotaka uwajibikaji kuhusu kauli hizo. Karua amemtetea mwanafunzi huyo akisema Bunge linapaswa kuwa […]

SERIKALI KUIMARISHA MCHAKATO WA KUWAJIRI POLISI

Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amesema serikali itaanzisha hatua kali zaidi katika mchakato wa kuajiri maafisa wa polisi ili kuimarisha nidhamu na weledi ndani ya huduma ya kitaifa ya Polisi. Hatua hiyo imefuatia kufukuzwa kwa makurutu 54 baada ya kubainika kuwa baadhi yao walikuwa na nyaraka za kughushi, hukumu za awali za uhalifu pamoja […]

RUTO AZINDUA KITUO CHA HUDUMA LAIKIPIA

Rais William Ruto amezuru Kaunti ya Laikipia ambapo amezindua mradi wa ujenzi wa kituo cha huduma katika eneo la Doldol ili kusogeza huduma za serikali karibu na wananchi. Rais ameahidi kuwa ujenzi wa barabara ya kilomita 60 kutoka Nanyuki kuelekea Doldol utaanza ndani ya wiki mbili zijazo, akiongeza kuwa serikali yake itajenga kilomita 217 zaidi […]

EUROPA: VILLA, FREIBURG KUMENYANA FAINALI, PALACE FAINALI CONF.

Klabu ya Aston Villa imesalia na mechi moja pekee kabla ya kutamatisha ukame wa kupata taji kuu kwa kipindi cha miaka 30, baada ya kutua fainali za kombe la UROPA League jana usiku kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Nottingham Forest. John McGinn alifunga mara mbili na kuongeza kwa bao la Emi Buendia la […]

AFCON 2027: KENYA YATANGAZA VIWANJA VITAKAVYOTUMIKA

Viwanja vya Kasarani na Talanta Sports City unaoendelea kujengwa ndivyo vitakavyotumika katika mashindano ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika, AFCON mwaka ujao, yatakayoandaliwa kwa pamoja katika mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania. Haya ni kulingana na katibu mkuu katika wizara ya michezo Elijah Mwangi, akisema uwanja wa Nyayo umewekwa katika kategoria ya viwanja mbadala, […]