ROONEY ONYANGO AITA AFCON 2027 FURSA YA KIPEKEE KWA KENYA

Beki wa kimataifa wa Kenya Rooney Onyango amesema mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2027 yatakuwa nafasi ya kipekee kwa soka ya Kenya kuandika historia mpya. Onyango ambaye kwa sasa anachezea Klabu Sogndal nchini Norway amesema mashindano hayo yatakuwa na uzito mkubwa kihistoria na kihisia kwa wachezaji wa Kenya. Beki huyo wa kulia mwenye umri wa […]

SERIKALI KUANZISHA MFUMO WA MIUNDOMBINU JULAI

Waziri wa Hazina ya Kitaifa John Mbadi amesema Mfuko wa Kitaifa wa Miundombinu utaanza kufanya kazi rasmi mwezi Julai mwaka huu kusaidia kufadhili miradi ya maendeleo nchini. Mbadi akiwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu kawi amesema baadhi ya miradi ya nishati imewekwa chini ya mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi. Aidha amesema baadhi ya miradi imehamishiwa […]

MARAGA AKOSOA SERIKALI KWA KUPUUZA MAAGIZO YA MAHAKAMA

Aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga ameikosoa serikali kwa kupuuza maagizo ya mahakama na kuahidi kulinda utawala wa sheria iwapo atachaguliwa kuwa rais. Akizungumza katika kaunti ya  Turkana Cwakati wa uzinduzi wa kampeni ya Ukombozi, Maraga amesema serikali ya sasa haiheshimu Katiba wala maamuzi ya mahakama. Amedai kuwa serikali imekuwa ikipuuzilia mbali maagizo ya fidia kwa wananchi waliojeruhiwa […]

VIONGOZI WA UASIN GISHU WATAKA ULINZI WA RAIS UIMARISHWE

Baadhi ya viongozi kutoka Kaunti ya Uasin Gishu wamekosoa hitilafu ya kiusalama iliyotokea wakati wa ziara ya Rais William Ruto katika Kaunti ya Kilifi. Viongozi hao wakiongozwa na Gavana wa Kaunti hiyo Jonathan Bii wametaka hatua zaidi kuchukuliwa kuimarisha usalama wa mkuu wa nchi. Wamesema ni muhimu kuhakikisha matukio kama hayo hayajirudii tena siku zijazo. Imetayarishwa na […]

STEPHEN MULE AKOSOA MFUMO WA UAGIZAJI MAFUTA

Mbunge wa Matungulu Stephen Mule amekosoa mfumo wa serikali kwa serikali wa uagizaji wa mafuta akitaka soko huria lirejeshwe. Mule pia amependekeza kupunguzwa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa mafuta kutoka asilimia 8 hadi 4 ili kupunguza mzigo kwa wananchi. Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja humu nchini, Mule amesema mfumo wa sasa umepunguza ushindani na kuchangia […]

RUTO ATAKA MAGEUZI YA HARAKA KATIKA UMOJA WA AFRIKA

Rais William Ruto ametaka kuharakishwa kwa mageuzi ndani ya Umoja wa Afrika ili bara la Afrika liweze kujitegemea zaidi kupitia taasisi imara na ufadhili endelevu. Rais amesema Afrika lazima ipunguze utegemezi wa nje na kuimarisha uwezo wake wa kushughulikia changamoto zake kupitia utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika. Ruto amezungumza baada ya kuongoza […]

MAANDAMANO YASHUHUDIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO NCHINI

Maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta nchini yamefanyka katika maeneo kadhaa nchini yakiwemo Roysambu, nyeri, Nyahururu miongoni mwa maeneo mengine. Waandamanaji hao wamefunga baadhi ya barabara na kuchoma magurudumu hali ilyolemaza shuguli za uchukuzi katika maeneo hayo huku polisi wakilazimika kutumia vitoa machozi kuwatanya waandamanaji hao waliokuwa wamefunga sehemu  ya barabra  kuu ya […]

MBADI  AWATAKA VIONGOZI WA UPINZANI KUSOMA NA KUUELEWA MSWADA WA FEDHA

Waziri wa fedha John Mbadi amewasuta vikali viongozi wa upinzani kwa madai ya kuwapotosha wakenya kuhusu mswada wa fedha wa 2026-2027. Akizungumza katika vikao na wanahabari jijini Nairobi, Waziri Mbadi amewataka viongozi haswa kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka  kukoma kuupotosha umma kuhusu baadhi ya vipengee vilivyomo ndani ya mswada huo. Imetayarishwa na Hilda […]

KINDIKI ASUTA VIONGOZI  WA SIASA WENYE MATAMSHI MABAYA

Naibu wa Rais Kithure Kindiki amejitenga na baadhi ya matamshi ya viongozi wa chama cha UDA kuwa wanalenga kuhitilafiana na matokeo ya Urais mwaka wa 2027 ili kumpa ushindi Rais William Ruto iwapo atapata kura chache katika uchaguzi mkuu ujao. Akijibu kauli ya viongozi  hao akiwemo  naibu wa gavana wa kaunti ya kakamega Ayubu Savula, […]

RAIS MUSTAAFU UHURU AONGOZA HAFLA YA CHAMA CHA JUBILLEE

Rais mustaafu Uhuru Kenyatta anaongoza mkutano wa wajumbe wa chama cha Jubilee katika kaunti ya Kiambu. Akizungumza kwenye hafla hiyo Uhuru amewashtumu wandani wa Rais William Ruto wanaomtaka astaafu katika ulingo wa siasa. Kulingana na Uhuru  tangu alipostaafu uongozini  mwaka wa 2022 chama chake kimekua kikikabiliwa na misukosuko akiapa kukiimarisha chama hicho. Imetayarishwa na Hilda […]