EPRA YAAHIRISHA MIKUTANO YA HADHARA KUHUSU MAPENDEKEZO MAPYA YA USHURU WA UMEME

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) imeahirisha vikao vya mashauriano vya umma nchini kote kuhusu mapendekezo ya ombi la bei ya reja reja ya umeme kwa mara ya tano kwa Udhibiti wa Ushuru wa mwaka wa kifedha 2026/27 hadi 2028/29. Katika notisi ya umma ambayo imetolewa, EPRA imetangaza kwamba mabaraza hayo, ambayo yalipangwa […]

CARRICK AONA NAFASI YA TATU KAMA MWANZO MPYA UNITED

Kocha wa Manchester United Michael Carrick amesema kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya uingereeza ni msingi mzuri wa kujenga mafanikio ya baadaye. Carrick alitoa kauli hiyo baada ya United kuhitimisha msimu kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion. Kocha huyo alithibitishwa rasmi kupewa kandarasi ya miaka miwili baada ya kuboresha […]

ARTETA SASA ALENGA UBINGWA WA ULAYA

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema sasa analenga kutwaa ubingwa wa UEFA Champions League baada ya kushinda Ligi Kuu ya uiingereza. Arteta alisema hayo baada ya Arsenal kusherehekea ubingwa kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika mechi ya mwisho ya msimu. Mabao ya Gabriel Jesus na Noni Madueke yaliihakikishia Arsenal kumaliza msimu ikiwa […]

KENYA YASHINDWA KUTAMBA CAPE TOWN MARATHON

Mashindano ya Sanlam Cape Town Marathon yalikuwa magumu kwa wanariadha wa Kenya huku nchi ikipata nafasi moja pekee ya jukwaani katika mbio za wanaume na wanawake. Kalipus Lomwai ndiye aliyekuwa Mkenya pekee kumaliza katika tatu bora baada ya kushika nafasi ya tatu kwa muda wa saa 2:05:06 katika mbio za wanaume. Mbio hizo zilitawaliwa na […]

OMANYALA BADO ANA NJAA YA MAFANIKIO ZAIDI

Mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika Ferdinand Omanyala amesema bado hajaridhishwa na mwanzo wake mzuri wa msimu wa mwaka 2026 huku akilenga mafanikio makubwa zaidi. Omanyala ameonyesha kiwango bora katika mashindano ya Diamond League nchini China ambapo aliibuka mshindi katika mbio za mita 100 kwa muda wa sekunde 9.94 mjini Xiamen. Mkenya huyo mwenye umri […]

ULINZI STARS WAPANIA KUEPUKA KUSHUKA DARAJA

Kocha wa Ulinzi Stars Mulinge Ndeto amesema timu hiyo itaendelea kupigania kusalia katika Ligi Kuu ya SportPesa hadi mwisho wa msimu. Kauli hiyo imejiri baada ya Ulinzi Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mathare United, ushindi uliowapa matumaini mapya ya kuepuka kushuka daraja. Timu hiyo sasa iko nafasi ya 15 ikiwa na […]

GOR MAHIA WATWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA FKF

Gor Mahia wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya FKF msimu wa 2025/26 baada ya AFC Leopards kufungwa mabao 2-1 na APS Bomet. K’Ogalo wameweka rekodi mpya kwa kutwaa taji lao la 22 licha ya kutocheza mechi yao dhidi ya Mara Sugar iliyositishwa kutokana na mzozo wa uwanja. Matokeo hayo yaliiacha AFC Leopards nyuma kwa alama […]

BUNGE LAPINGA TAARIFA ZA USHURU KWA ARDHI YA UMILIKI WA KUDUMU

Bunge la Kitaifa limekanusha taarifa zinazosambazwa mtandaoni kuwa Mswada wa Fedha 2026 unapendekeza Wakenya kulipa kodi ya kila mwaka kwa ardhi ya umiliki wa kudumu. Bunge hilo limesema madai hayo ni ya kupotosha na yanalenga kuwachanganya wananchi kuhusu yaliyomo kwenye mswada huo. Limefafanua kuwa Mswada wa Fedha 2026 hauna kipengele chochote kinachohusu ushuru wa ardhi, umiliki wa kudumu wala […]

BAADHI YA VIONGOZI WA ODM WAUNGA MKONO SERIKALI JUMUISHI

Baadhi ya viongozi wa Chama cha ODM wanaounga mkono serikali jumuishi wamesema wataendelea kushirikiana na serikali baada ya kuwa muda mrefu katika upinzani. Viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama Gladys Wanga wamesema ushirikiano na serikali utasaidia maeneo yao kupata maendeleo na kunufaika zaidi. Wamewahimiza wafuasi wao kuunga mkono serikali huku baadhi wakipendekeza kuwepo kwa utaratibu wa […]

VIONGOZI WA KENYA KWANZA WAONYESHA IMANI KWA RUTO 2027

Baadhi ya viongozi wa Muungano wa Kenya Kwanza wameeleza imani kuwa Rais William Ruto atapata muhula wa pili kutokana na rekodi yake ya maendeleo na juhudi za kuunganisha taifa. Wakizungumza katika eneo bunge la Turbo, Viongozi hao Wamedai kuwa viongozi wa upinzani wanaendeleza siasa za mgawanyiko badala ya kuangazia maendeleo ya wananchi. Aidha wamemtetea Rais kuhusiana […]