METTE AJIWEKEA MALENGO MAKUBWA KWENYE KOMBE LA CECAFA KAGAME
Kocha wa Tusker, Julien Mette, amesema analenga kuunda kikosi imara kitakachowania ubingwa wa Kombe la CECAFA Kagame litakalofanyika mjini Kigali, Rwanda, kuanzia Julai 24.
Mfaransa huyo amesema ameweka mikakati ya kuhakikisha mabingwa wa Kombe la Mozzart Bet wanatoa ushindani mkubwa dhidi ya timu bora kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.
Tusker ilipata nafasi ya kushiriki mashindano hayo baada ya klabu ya Al Merreikh ya Sudan kujiondoa, hatua iliyofungua fursa kwa wawakilishi hao wa Kenya kupima uwezo wao katika mashindano ya kikanda.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































