USHINDI WA DCP OL KALOU WABADILISHA MWELEKEO WA SIASA ZA MLIMA KENYA
Ushindi mkubwa wa DCP katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou umeongeza uzito wa ushindani wa kisiasa katika eneo la Mlima Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.
Kwa Rais William Ruto, matokeo hayo yanatazamwa na wachambuzi wa kisiasa kuwa yanazua maswali kuhusu nguvu ya ushawishi wa kisiasa wa chama chake katika eneo hilo, hasa baada ya kuongoza kampeni za mgombea wa UDA pamoja na viongozi wengine wa serikali.
Kwa upande wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, ushindi huo unaipa DCP kiti chake cha kwanza bungeni na kuimarisha hoja yake kwamba bado ana ushawishi mkubwa wa kisiasa katika eneo la Mlima Kenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































