HANSEL OCHIENG’ AWEKA MALENGO MAKUBWA GOR MAHIA
Mshambuliaji mpya wa Gor Mahia, Hansel Ochieng’, amesema lengo lake la kwanza ni kuisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya FKF katika msimu wa 2026/27.
Ochieng’ pia amesema anatamani kuifikisha Gor Mahia hatua za juu za Ligi ya Mabingwa barani Afrika na kuchangia mafanikio ya klabu hiyo kimataifa.
Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa Kenya baada ya kujiunga kutoka APS Bomet, akiwa pia amewahi kuzichezea AFC Leopards, Kakamega Homeboyz na Nairobi City Stars.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































