#Football #Sports

GOR MAHIA YAZINDUA KAMPENI YA KUCHANGISHA FEDHA KWA MASHABIKI

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu ya FKF, Gor Mahia, wamezindua kampeni mpya ya kuchangisha fedha kwa ushirikiano na wadhamini wao, Kansai Plascon Kenya, kuelekea ushiriki wao katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika

Kupitia mpango unaoitwa Wallcover K’Ogalo Edition, sehemu ya mapato yatokanayo na mauzo ya rangi maalumu yatatumika kufadhili maandalizi ya klabu kwa msimu wa 2026/27 wa mashindano hayo.

Kampeni hiyo inawapa mashabiki nafasi ya kuchangia moja kwa moja maandalizi ya timu, huku makopo ya rangi yakibeba rangi za kijani na nyeupe pamoja na michoro inayoadhimisha historia na mafanikio ya Gor Mahia nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *