RUTO: UCHAGUZI USIGAWANYE WAKENYA
Rais William Ruto amewataka Wakenya kutoruhusu uchaguzi kuwa chanzo cha migawanyiko, akisema kuwa ushindani wa kisiasa ni wa muda lakini umoja wa taifa unapaswa kudumu.
Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi alipokutana na viongozi wa mashinani kutoka Kaunti ya Bungoma wakiongozwa na Mbunge wa Kimilili, Didmus Barasa, Rais amesema uchaguzi haupaswi kuchukuliwa kama suala la uhai au kifo.
Aidha, amewatahadharisha wanasiasa dhidi ya kuwagawa wananchi kwa misingi ya ukabila na kuwahimiza kuendeleza mshikamano wa kitaifa pamoja na kuelekeza juhudi katika kuboresha maisha ya Wakenya badala ya siasa za mgawanyiko.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































