#Local News

METHU AIPONGEZA IEBC KWA KUSIMAMIA UCHAGUZI WA OL KALOU

Seneta wa Nyandarua, John Methu, ameipongeza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa jinsi ilivyosimamia uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou.

Methu amesema ameridhishwa na huduma zilizotolewa na tume hiyo wakati wa mchakato wa uchaguzi, akieleza kuwa uchaguzi umeendeshwa kwa mafanikio.

Wakati huohuo Methu amekashifu visa vya vurugu na uhuni vilivyotokea akisema kuwa kuna haja ya kuwepo na amani nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *