#Business

GIZA LATANDA SOKO LA MARIKITI JIJINI NAIROBI KWA KUKOSA UMEME

Wafanyabiashara katika soko kubwa la marikiti jijini Nairobi wanaendelea kukadiria hasara baada ya kampuni ya umeme nchini KPLC kukata umeme katika soko hilo kufuatia deni kubwa linalodaiwa na kampuni ya umeme kutoka kaunti ya Nairobi.

Wanabiashara hao sasa wanataka usimamizi wa kaunti ya Nairobi kuwajibika na kuleta suluhu ya haraka ili kulinda uchumi wa nchi kwani wametaja kuwa soko la marikiti linategemewa kwa biashara nyingi mno na familia nyingi mno ndani nan je ya jiji la Nairobi.

Hata hivyo, baadhi ya wafanyibiashara katika soko hilo wamesema kuwa kama wachuuzi wanalipa ushuru kulingana na kanuni za kaunti ya Nairobi ni vyema serikali kuu kuingilia kati na kuleta suluhu katika soko hilo na kuwaokoa wafanyibiashara ambao ni walipa ushuru.Ikumbukwe kwamba kampuni ya kusambaza umeme nchini hapo awali ilirundika lori ya taka katikati mwa jiji la Nairobi kufuatia deni ililokuwa ikidai kaunti ya Nairobi kwa muda.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *