#Local News

SAMMY WAWERU ASHINDA KITI CHA OL KALOU 

Mgombea wa chama cha DCP, Sammy Douglas Waweru Kamau, amechaguliwa kuwa Mbunge mpya wa Ol Kalou baada ya kuibuka mshindi kwa tofauti kubwa ya kura dhidi ya mpinzani wake wa karibu.

Matokeo rasmi yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) yanaonyesha kuwa Waweru alipata zaidi ya kura 35,440, huku mgombea wa UDA, Samuel Muchina Nyagah, akipata takriban kura 5,450.

Ushindi huo unaipa DCP kiti chake cha kwanza bungeni tangu kuanzishwa kwa chama hicho, huku ukitafsiriwa na wachambuzi wa siasa kama matokeo yenye uzito mkubwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *