#Local News

UDA YAPUUZA KUSHINDWA OL KALOU

Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kimesema kushindwa kwake katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou hakupunguzi ushawishi wa chama hicho katika eneo la Mlima Kenya wala uungwaji mkono kwa serikali ya Rais William Ruto.

Akizungumza na wanahabari, Katibu Mkuu wa UDA, Hassan Omar, amewapongeza mgombea mshindi na aliyeshindwa, huku akiwashukuru wakazi wa Ol Kalou kwa kushiriki uchaguzi kwa amani na kutumia haki yao ya kidemokrasia.

Aidha, Hassan Omar amesema chama hicho kitaendelea kuimarisha shughuli zake za kisiasa na kushirikiana na wananchi katika kutekeleza ajenda zake za maendeleo nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *