JULIUS YEGO ALENGA KUMALIZA KWA FAHARI MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA
Bingwa wa dunia wa kurusha mkuki mwaka 2015, Julius Yego, amesema analenga kumaliza safari yake ya Michezo ya Jumuiya ya Madola kwa mafanikio wakati mashindano hayo yatakapoanza wiki ijayo mjini Glasgow, Scotland.
Yego, ambaye sasa ni mmoja wa wanariadha wenye uzoefu mkubwa nchini, atashiriki mashindano hayo kwa mara ya nne tangu aanze mwaka 2010 mjini New Delhi, India.
Mwanariadha huyo amesema bado anaamini ana uwezo wa kutupa umbali mkubwa msimu huu na ameahidi mashabiki wake kuwa atajitahidi kuleta matokeo bora katika mashindano hayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































