#Local News

SIFUNA AONDOLEWA NAFASI YA NAIBU MJELEDI WA WACHACHE SENETI

Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ameondolewa katika wadhifa wa Naibu Kiranja wa Wachache katika seneti Seneti kufuatia hatua mpya ya chama cha ODM dhidi yake.

Katika taarifa iliyowasilishwa bungeni na Spika wa Seneti Amason Kingi, Seneta wa Migori Eddy Oketch alitangazwa mara moja kuchukua nafasi hiyo.

Mabadiliko hayo yamekuja baada ya mkutano wa maseneta ulioripotiwa kufanyika katika ofisi ya Kiranja wa Wachache Ledama Ole Kina, huku uamuzi huo ukiendelea kupingwa na kiongozi wa Azimio Kalonzo Musyoka.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *