#Local News

GACHAGUA AMSUTA IG KANJA NA IEBC BAADA YA UCHAGUZI WA OL KALOU

Kiongozi wa chama cha DCP, Rigathi Gachagua, amemsuta Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kwa madai ya kuhusika na vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou.

Katika taarifa yake, Gachagua amedai kuwa baadhi ya maafisa wa usalama walitumiwa kuwatisha wapigakura na kuathiri mchakato wa uchaguzi, madai ambayo hayajathibitishwa na mamlaka husika.

Aidha, ameiikosoa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kile alichodai ni ukimya wake wakati wa madai ya ukiukaji wa haki za wapigakura katika uchaguzi huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *