#Local News

PASSARIS AWATAKA VIJANA KUKATAA KUTUMIWA KISIASA

Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Nairobi, Esther Passaris, amewataka vijana kuepuka kutumiwa na wanasiasa kushiriki vitendo vya uhuni na vurugu.

Akizungumza jijini Nairobi, Passaris amesema vijana wanapaswa kushiriki katika shughuli za maendeleo badala ya kuhusishwa na fujo za kisiasa.

Aidha, amewahimiza vijana kumuunga mkono Rais William Ruto, akisema kuwa miradi na mipango ya maendeleo ya serikali yake inaendelea kuwanufaisha wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

PASSARIS AWATAKA VIJANA KUKATAA KUTUMIWA KISIASA

UDA YAPUUZA KUSHINDWA OL KALOU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *