AFISA ALIYE UAWA HAITI ATAMBULIWA
Afisa wa polisi wa kikosi cha Kenya aliyefariki kwenye ajali mbaya ya barabarani Jumapili nchini Haiti ametambuliwa kama Koplo Kennedy Mutuku, mweye umri wa miaka 41.
Cue in Shadrack Maina
Kupitia taarifa, kikosi cha Pamoja cha mataifa mbali mbali kinachoendesha operesheni ya amani nchini humo MSS, kimemtaja Mutuku kuwa afisa shupavu wa kikosi cha 3 cha Kenya, ambaye amehudumu katika Idara ya polisi tangu mwaka wa 2005.
Licha ya operesheni ya usalama, mashirika ya kimataifa yamesema hali ya usalama ingali tete, huku baraza la mpito likiahidi kuandaa uchaguzi kabla ya Februari mwaka ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































