#Local News

NTSA YAFUTILIA MBALI LESENI ZA MADEREVA 62

Mamlaka ya kitaifa inayosimamia usalama barabarani NTSA imefutilia mbali leseni za madereva 62 kutoka kampuni 7 za magari ya uchukuzi wa umma baada ya ukaguzi uliobaini kuwa madereva hao wamekiuka sheria za usalama.

Kupitia taarifa, NTSA imesema madereva hao watahitajika kufanya majaribio mapya ya uendeshaji wa magari kabla ya kuamuliwa iwapo watarejeshewa leseni zao au la.

Aidha, mamlaka hiyo imeziagiza kampuni zilizoathirika kuwapa madereva wao wote uhamasisho kuhusu usalama wa barabarani.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *