GEORGE KAMAL AMRITHI KILAVUKA KQ
Shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) limemteua Kapteni George Kamal kama Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa na Afisa Mkuu Mtendaji kufuatia kuondoka kwa Allan Kilavuka ambaye muda wake wa kuhudumu ulikamilika.
Katika taarifa yake, Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo la ndege imesema Kilavuka ataendelea na likizo ya mwisho kabla ya kumalizika kwa mkataba wake, kuashiria mwisho wa miaka sita ya uongozi wa shirika la ndege la kitaifa.
Kamal, ambaye kwa sasa anahudumu kama Afisa Mkuu wa Uendeshaji, alichukua nafasi hiyo ya Kaimu Mtendaji Mkuu kuanzia jana mwezi, bodi inapoanza mchakato wa kuajiri mtendaji mkuu mashuhuri.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































