NATEMBEYA AIBUKA MAARUFU MAGHARIBI
Ulingo wa kisiasa Magharibi mwa Kenya umechukua mkondo tofauti, utafiti ukionyesha kuwa wenyeji sasa wamewaasi viongozi wa siku nyingi eneo hilo na kuwakumbatia viongozi wa kizazi kipya.
Kulingana na matokeo ya utafiti wa shirika la Infotrak yaliyotolewa hapo jana kuhusu umaarufu wa viongozi wa eneo hilo, gavana wa Trans Nzoia George Natembeya anapendelewa na asilimia 32 ya wakazi, akiwapiku spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula na mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi.
Kwenye utafiti huo wa mwezi jana, seneta wa Nairobi Edwin Sifuna pia amepata umaarufu zaidi eeno hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































