#Local News

GACHAGUA ATAKA SERIKALI KUTANGAZA UKAME JANGA LA KITAIFA.

Kinara wa DCP Rigathi Gachagua sasa anataka serikali itangaze hali ya ukame nchini kuwa janga la kitaifa.

Akizungumza na wanahabari, Gachagua amesema eneo la kaskazini mwa Kenya lililoathirika zaidi linahitaji msaada wa dharura.

Gachagua Pia amewalaumu viongozi wa kaskazini mashariki kwa kusalia kimya, licha ya ukame kumaliza mifugo na kuathiri wakaazi wake.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *