MAHAKAMA YAAGIZA KUACHILIWA KWA MWAGODI MWABILI
Mahakama moja jijini Nairobi imetoa uamuzi wa pande mbili kuhusiana na maombi yaliyowasilishwa kuhusu uchunguzi na kuzuiliwa kwa mwanaharakati Mwagodi Mwabili.
Katika ombi la kwanza, mahakama iliruhusu Idara ya Upelelezi wa Jinai kuendelea kushikilia simu ya mkononi ya Mwabili kwa ajili ya uchunguzi zaidi, ikisema kifaa hicho ni muhimu kama kielelezo katika uchunguzi wa machapisho yake kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Hata hivyo, katika ombi la pili, mahakama ilikataa ombi la Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka la kuendelea kumzuilia mwanaharakati huyo na ikaamuru aachiliwe mara moja, ikieleza kuwa hakuna msingi wa kuendelea kumweka rumande kwa sasa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































