#Sports

MADEREVA 18 WA KENYA KUSHIRIKI SAFARI RALLY NAIVASHA

Madereva 18 wa Kenya na wasaidizi wao 14 watakuwa miongoni mwa magari 46 yatakayoshiriki katika mashindano ya WRC Safari Rally Kenya, yatakayofanyika kuanzia Machi 12 hadi 15 mjini Naivasha. Mashindano hayo pia yatakuwa duru ya kwanza ya Kenya National Rally Championship.

Safari Rally ya mwaka huu itakuwa duru ya tatu kati ya 14 za mfululizo wa World Rally Championship, huku washiriki wakikabiliwa na siku nne za mashindano makali katika ardhi yenye changamoto kuzunguka Ziwa Naivasha.

Miongoni mwa watakaoshiriki ni bingwa wa zamani wa Kenya Jasmeet Chana, Pauline Sheghu na Lisa Christoffersen. Pia, bingwa mara mbili wa Afrika katika mashindano ya magari, Karan Patel, ataungana na Tauseef Khan wakitumia Skoda Fabia, huku bingwa mara tano wa Safari Rally Carl Tundo akiungana na Tim Jessop wakitumia Ford Fiesta.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuleta ushindani mkali kati ya madereva chipukizi na wakongwe wa Kenya dhidi ya nyota wa kimataifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *