UTATA WA PASPOTI MIKONONI MWA RAIA WA KIGENI
Idara ya uhamiaji inatarajiwa kutoa taarifa kuhusu madai ya kukiuka sheria na kutoa paspoti za usafiri kwa raia wa kigeni wanaohusishwa na Sakata za ufisadi na mapigano , akiwemo Algoney Dagalo Hamdan, kakake mdogo wa kiongozi wa kundi la wapiganaji nchini Sudan RSF, Mohammed Hamdan.
Wengine walio na paspoti hizo ni raia wa Sudan wanaoaminika kuwa watu wa karibu na Hamdan, ambao ni Mayada Hamdan, Abdaraheem Hamdan, Musa Hamdan, Zahra Hamdan na Zariwa Hamdan.
Awali, naibu rais wa zamani Rigathi Gachagua aliibua madai kwamba makamanda wa RSF wanamiliki stakabadhi hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































