SIFUNA: HAKUTAKUWA NA KUONGEZWA KWA MKATABA WA UDA NA ODM
Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amekanusha uwezekano wowote wa kuongezwa kwa Mkataba wa Maelewano kati ya chama cha UDA na ODM baada ya tarehe ya mwisho ya Machi 7.
Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga humu nchini, Sifuna amesema makubaliano hayo yaliyotiwa saini Machi 7, 2025, hayakuwa na kipengele chochote cha kuongezwa muda, na yalipangwa kudumu hadi Machi 7, mwaka huu pekee.
Aidha amesitiza kuwa hakuna afisa mwingine wa chama aliye na mamlaka ya kubadilisha au kuongeza muda wa makubaliano hayo, akieleza kuwa Hayati Raila Odinga aliunda mkataba huo kimakusudi bila kipengele cha kuongezwa muda.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































