#Rugby #Sports

KCB RFC, KABRAS RFC WAGAWANA HASARA YA MVUA

Klabu za raga KCB RFC na bingwa mtetezi Kabras RFC zililazimika kukubali sare ya 10-10 baada ya mechi kati yao kukatizwa na mvua nyingi iliyosababisha maji mengi katika uwanja wa KCB Sports Club Ruaraka.

Mechi hiyo ya Kenya Cup iliyokuwa imewaleta pamoja miamba 2 wa raga ambao hawajapoteza mechi msimu huu, ilikuwa imepigiwa upato kuwa mechi ya aina yake.

Hata hivyo, mvua iliyonyesha bila kikomo ilisababisha kutuama kwa maji uwanjani na kuwatatiza wachezaji, timu zote zikishindwa kutekeleza mipango yao.

KCB walianza kwa kishindo, ila Brian Wahinya akapoteza penalti ambayo ingewapa wenyeji uongozi, ingawa alifuta makosa yake na kufunga penalti nyingine na kuwaweka kifuo mbele 3-0.

Fidel Maina alifunga trai nyingine kabla ya Wahinya kufanya mambo kuwa 10-0.

Kabras walijibu kabla ya mechi kusitishwa, Eric Cantona akifunga penalti baada ya trai ya awali na kufanya mambo kuwa 10-10.

Hata hivyo, ongezeko la mvua liliwaacha waandalizi bila njia mbadala isipokuwa kukatiza mechi hiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KCB RFC, KABRAS RFC WAGAWANA HASARA YA MVUA

BB BREAD YABOMOA GOR, AFC LEOPARDS

KCB RFC, KABRAS RFC WAGAWANA HASARA YA MVUA

DROO YA ROBO FAINALI YA FA CUP

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *