#Sports

BROOKSIDE YADHAMINI MICHEZO YA SHULE

Kampuni ya Brookside Dairy imetoa shilingi milioni 30 kudhamini michezo ya kitaifa ya shule za upili ya muhula wa kwanza ya mwaka 2026 itakayofanyika katika Shule ya Kisumu kuanzia Aprili 5 hadi 11.

Fedha hizo zitalenga kusaidia maandalizi na uendeshaji wa mashindano hayo yanayokutanisha timu bora zilizofuzu kutoka ngazi za kanda na mikoa, huku michezo kama riadha, mpira wa kikapu, magongo na raga ya wachezaji 15 ikishirikishwa.

Akizungumza jijini Nairobi wakati wa uzinduzi, Meneja wa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Wilson Okong’o, amesema udhamini huo unaonyesha kujitolea kwa muda mrefu katika kukuza vipaji vya vijana kupitia michezo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *