ODM YAANZISHA MCHAKATO WA KUMTIMUA SIFUNA
Katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna ana siku 4 kupinga kutimuliwa kwake kutoka wadhifa huo huku akitakiwa kufika mbele ya kamati ya nidhamu ya chama hicho tarehe 10 mwezi huu.
Kupitia waraka uliotiwa saini na mwenyekiti Gladys Wanga, ODM imemtuhumu Sifuna na mashtaka 5, ikiwemo madai ya kukiuka msimamo wa chama kuhusu ushirikiano na UDA, kubuni mrengo pinzani wa Linda Mwananchi, na kupuuza uamuzi wa baraza kuu la chama hicho.
Sifuna amewateua mawakili tajika watatu kumwakilisha kwenye kesi hiyo, ingawa ODM imepinga uteuzi huo kwa misingi kwamba ni jukumu la kamati simamizi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































