MAWAZIRI WACHUNGUZWA KATIKA SAKATA YA MAFUTA
Mawaziri wawili ni miongoni mwa wanaochunguzwa kuhusiana na sakata ya mafuta ya shilingi bilioni 4.8 iliyosababisha kukamatwa na kujiuzulu kwa wakuu watatu wa sekta ya kawi.
Sakata hiyo inahusisha uingizaji wa shehena mbili za petroli zenye uzito wa tani 128,000 nje ya makubaliano ya kiserikali ya ununuzi wa moja kwa moja, ambapo serikali hununua mafuta kutoka Saudi Arabia na Falme za Kiarabu.
Barua mbili zilizofichuliwa zimewataja Opiyo Wandayi na Lee Kinyanjui kuhusiana na mchakato huo, Wawili hao sasa wakitarajiwa kuwasilisha maelezo yao kwa DCI kuhusu sakata hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































