KICD YAAGIZA TAKWIMU ZA WANAFUNZI WA GREDI YA 10
Taasisi ya Ukuzaji Mitaala nchini imeagiza wakuu wa shule zote za umma za upili kuwasilisha takwimu za wanafunzi wa Gredi ya kumi ili kuandaa hatua inayofuata ya ugavi wa vitabu vya masomo.
Mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo, Charles Ng’ondo, amekiri kuwepo kwa mapungufu ambapo baadhi ya shule zina vitabu vingi kupita kiasi huku nyingine zikiwa hazijapokea hata kimoja, hali inayotokana na tofauti ya takwimu za awali na idadi halisi ya wanafunzi pamoja na masomo wanayochagua.
Taasisi hiyo imesema mchakato huo unalenga kutekeleza sera ya serikali ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata kitabu chake binafsi kwa kila somo, huku awamu ya pili ya ugavi ikikusudiwa kufanikisha lengo hilo kikamilifu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































