#Local News

MATUMIZI YA FEDHA IKULU YAWASHANGAZA WACHANGANUZI

Hofu imeibuliwa kuhusu ongezeko la matumizi ya fedha katika afisi ya Rais William Ruto, ikibainika kuwa kufikia mwezi Juni mwaka huu, afisi hiyo itakuwa imetumia takribani shilingi bilioni 100, kiasi cha fedha zinazotumika kuendesha afisi yake, ile ya naibu rais, afisi ya mkuu wa mawaziri na wizara mbali mbali.

Kwa mujibu wa takwimu, kuna ongezeko kubwa katika matumizi ya fedha katika afisi ya urais chini ya Rais Ruto, ikilinganishwa na mtangulizi wake Uhuru Kenyatta aliyetumia takribani shilingi bilioni 90 katika kipindi chote cha miaka 10.

Wachanganuzi wa masuala ya kiuchumi sasa wameshnikiza uwazi kuhusiana na matumizi ya fedha katika Ikulu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MATUMIZI YA FEDHA IKULU YAWASHANGAZA WACHANGANUZI

MIANYA YA UFADHILI WA MASOMO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *