IEBC YATOA TARAIFA KUHUSU USAJILI WA WAPIGA KURA
Zoezi la usajili wa wapiga kura wapya limeratibiwa kukamilika hii leo huku tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC ikisema inajitahidi kuwafikia wakenya wote waliohitimu ili kuwasajili kabla ya zoezi hilo kufungwa.
Katika taarifa ya hivi punde, IEBC imesema imeafikia asilimia 75 ya wapiga kura wapya milioni 2.5 waliokuwa wamelengwa, Nairobi ikiongoza kwa takribani wapiga kura wapya zaidi ya 200,000.
Tume hiyo imetangaza kuwa imewasajili wapiga kura milioni 1.8 kufikia jana kwenye zoezi lililoanza tarehe 30 mwezi jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































