KESI YA GACHAGUA KUENDELEA MEI 22
Kesi ya kushinikiza fidia kwa aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua itaendelea Ijumaa wiki ijayo huku naibu Rais Kithure Kindiki akiiomba mahakama kutupilia mbali kesi hiyo ambapo Gachagua anataka kupewa malipo ya muhula mzima ambayo angepokea iwapo hangetimuliwa kutoka afisini.
Kupitia kwa wakili wake, Kindiki amesema kulipwa fidia kwa mtangulizi wake kutahujumu uamuzi wa seneti kumwondoa mamlakani.
Hata hivyo, mawakili wa Gachagua wamesisitiza kuwa mchakato wa kumtimua mteja wao ulikiuka sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































