WAFCON: HARAMBEE STARLETS KUHAKIKISHIWA SHILINGI MILIONI 19.5
Harambee Starlets imehakikishiwa angalau shilingi milioni 19.5 baada ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026, kufuatia ongezeko la zawadi lililotangazwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
CAF imesema kila moja ya mataifa 16 yatakayoshiriki mashindano hayo itapokea dola 150,000, sawa na shilingi milioni 19.5, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ikilinganishwa na toleo lililopita.
Aidha, CAF imeongeza jumla ya kitita cha zawadi kwa asilimia 67, kutoka dola milioni 3.475 hadi dola milioni 5.8, hatua inayofanya WAFCON 2026 kuwa mashindano yenye zawadi kubwa zaidi katika historia yake.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































