LSK YASISITIZA KUENDELEZA MGOMO WAO
Chama cha Wanasheria nchini, LSK, kimethibitisha kuwa mgomo wake wa kutoshiriki katika shughuli za mahakama bado unaendelea kote nchini, huku kikitoa wito kwa mawakili wote kuendelea kususia vikao vya mahakama ili kushinikiza uwajibikaji zaidi ndani ya Idara ya Mahakama.
Akizungumza hii leo nje ya Mahakama ya Juu, Rais wa LSK, Charles Kanjama, amesema mgomo huo unaendelea kuzingatiwa katika maeneo mbalimbali nchini na kuwahimiza wanachama wote kuendelea kutekeleza agizo hilo.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































