WANASHERIA KUGOMA JUMATANO
Idara ya Mahakama imesema mahakama zote nchini zitafunguliwa kama kawaida Jumatano licha ya Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) kutangaza kususia baadhi ya shughuli za mahakama.
LSK imesema mawakili wake hawatahudhuria kesi zitakazosimamiwa na majaji wanaodaiwa kuzuia uchunguzi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama (JSC) na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuhusu malalamishi dhidi yao.
Hata hivyo, Idara ya Mahakama imewahakikishia Wakenya kuwa huduma zote zitaendelea kutolewa kama kawaida, huku ususiaji huo ukitarajiwa kuathiri baadhi ya kesi katika mahakama mbalimbali.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































