#Local News

VIONGOZI WA BROAD-BASED WAPUUZA MATOKEO YA OL KALOU

Viongozi wa serikali ya muungano mpana wamepuuza ushindi wa chama cha DCP katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou, wakisema sio taswira kamili ya kisiasa nchini kwa ujumla.

Wakizungumza katika kaunti mbalimbaliviongozi hao wamesema Rais William Ruto bado anaungwa mkono na wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Viongozi hao pia wamemtaka Kinara wa DCP Rigathi Gachagua na washirika wake kutojipa matumaini makubwa kutokana na ushindi huo, wakisisitiza kuwa ushindani wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 bado uko mbali.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

VIONGOZI WA BROAD-BASED WAPUUZA MATOKEO YA OL KALOU

WANASHERIA KUGOMA JUMATANO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *