JAJI MKUU KOOME ATAKA MATUMIZI YA UJASUSI KUKABILI UHUNI
Jaji Mkuu Martha Koome amesema vitendo vya uhuni vinaweza kuzidi uwezo wa polisi kukusanya ushahidi na kuwafikisha wahusika mahakamani, hasa vinapohusisha makundi makubwa ya watu.
Koome amesema ni muhimu kwa vyombo vya usalama kutumia mbinu za kijasusi pamoja na mikakati mingine ya mapema ili kuwabaini wahusika na kuzuia matukio hayo kabla hayajatokea.
Aidha, amesisitiza kuwa hatua za kuzuia uhalifu mapema ni muhimu katika kuimarisha usalama wa wananchi na kuhakikisha wahalifu wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































