#Local News

DPP YAKARIBISHA HUKUMU DHIDI YA OBADO

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Ingonga amepongeza uamuzi wa Mahakama Kuu uliowapata na hatia aliyekuwa Gavana wa Migori, Okoth Obado, pamoja na Michael Oyamo na Caspal Obiero katika kesi ya mauaji ya Sharon Otieno.

Katika taarifa yake, DPP amesema sasa inasubiri mahakama kutoa adhabu inayostahili, akieleza matumaini kuwa hukumu hiyo itakuwa ya kuzuia uhalifu na kuakisi uzito wa kosa lililotendwa.

Aidha, DPP imesema kutiwa hatiani kwa washtakiwa hao ni hatua muhimu katika kuimarisha uwajibikaji na kuhakikisha waathiriwa wa uhalifu mkubwa wanapata haki kwa mujibu wa sheria.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *