#Local News

GACHAGUA AAHIDI MAGEUZI KATIKA VITENGO VYA POLISI

Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema kipaumbele chake cha kwanza akichaguliwa kuwa Rais kitakuwa kuwaondoa maafisa wa polisi anaodai wanahusika katika vitendo vya uhuni wa kisiasa.

Akizungumza katika mazishi ya wafuasi wawili wa DCP waliofariki siku ya uchaguzi mdogo wa Ol Kalou, Gachagua pia amewaonya machifu na manaibu wa machifu dhidi ya kujihusisha na siasa za upendeleo.

Aidha, alimkosoa Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen, akisema kauli yake ya kukabiliana na wahuni haina uhalali kwa madai kuwa baadhi ya vitendo hivyo vinafanyika chini ya usimamizi wa wizara hiyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *