#Local News

SEKTA YA USAFIRI WA ANGA YAKABILIWA NA TISHIO LA MGOMO

Sekta ya usafiri wa anga nchini inakabiliwa na tishio la mgomo baada ya Muungano wa Wafanyakazi wa Usafiri wa Anga Kenya (KAWU) kutoa ilani ya siku saba ya kusitisha kazi.

Mgomo huo unatarajiwa kuwaathiri wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya (KCAA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya (KAA), Kenya Airways na Jambojet.

Muungano huo umesema uamuzi huo umechochewa na migogoro ya muda mrefu ya kikazi, ikiwemo kucheleweshwa kwa utekelezaji wa mikataba ya pamoja ya wafanyakazi pamoja na wasiwasi kuhusu usalama wa ajira.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *