OMIJA ASEMA MCCARTHY ALICHANGIA PAKUBWA KWENYE UHAMISHO WAKE
Beki wa Harambee Stars, Alphonce Omija, amesema kocha Benni McCarthy alichangia pakubwa uhamisho wake kwenda klabu ya Étoile Sportive du Sahel ya Tunisia, hatua anayoiita mafanikio makubwa zaidi katika maisha yake ya soka.
Omija alivutia vilabu mbalimbali baada ya kung’ara akiwa na Gor Mahia na baadaye kuonyesha kiwango bora katika mashindano ya CHAN 2024, hali iliyomfanya kuwindwa na klabu kutoka Afrika Kusini na Sudan.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 amesema alikataa ofa ya awali kutoka Durban City baada ya kushauriwa na McCarthy kutohudhuria majaribio katikati ya mashindano, ushauri uliomfungulia njia ya kutua nchini Tunisia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































