#Local News

MLA WATU AWAUMA NA KUWAIBIA WAKAAZI WA RUIRU

Wakazi wa eneo la Gitothua mjini Ruiru wamekumbwa na hofu kufuatia msururu wa mashambulizi ya usiku yanayodaiwa kufanywa na mtu asiyejulikana anayewashambulia watembea kwa miguu, kuwaibia na kisha kuwauma.

Wakazi wanasema matukio hayo yameongezeka katika mwezi wa Julai na kuwafanya wengi kuepuka kutembea nje wakati wa usiku kutokana na hofu ya kushambuliwa na mtu huyo

Katika moja ya mashambulizi hayo, mwathiriwa mmoja alijeruhiwa vibaya usoni baada ya mshukiwa kudaiwa kumuuma na kung’oa sehemu ya shavu lake, wakazi sasa wakitaka vyombo vya usalama kuchukua hatua za haraka kumkamata mhusika na kurejesha usalama katika eneo hilo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *