#Local News

VIONGOZI KUTOKA PWANI WAKEMEA KAULI ZA GACHAGUA KUHUSU UTALII

Serikali, wadau wa utalii na viongozi wa eneo la Pwani wamekosoa kauli za aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua zinazodaiwa kuhimiza watalii wa kimataifa kususia kutembelea Kenya.

Shirikisho la Utalii Kenya limesema kauli hizo zinaweza kudhoofisha imani ya wawekezaji na watalii, likiwataka kupuuza matamshi hayo na kuendelea kuunga mkono sekta ya utalii nchini.

Nao Mawaziri Ali Hassan Joho na Salim Mvurya wamemsuta Gachagua kwa madai ya kujaribu kuwagawa Wakenya na kuhujumu sekta ya utalii, wakisisitiza kuwa utalii unasalia kuwa nguzo muhimu ya uchumi wa eneo la Pwani na taifa kwa ujumla.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *