CHETI CHA POLISI SASA KUTOLEWA NDANI YA SIKU MOJA
Wananchi sasa wataweza kupata cheti cha kutokuwa na rekodi ya uhalifu ndani ya siku moja kufuatia uzinduzi wa mfumo mpya wa utambuzi wa kibayometriki unaolenga kuharakisha uchunguzi wa makosa ya jinai nchini.
Hatua hiyo pia imeifanya Kenya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata ithibati ya kimataifa kwa mfumo wake wa usimamizi wa vielelezo vya uchunguzi wa kisayansi wa polisi, hatua inayolenga kuimarisha utoaji wa haki.
Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amesema maendeleo hayo ni hatua muhimu katika kuimarisha matumizi ya teknolojia katika kazi za polisi na kuboresha ufanisi wa uchunguzi wa uhalifu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































