#Football #Sports

MARVIN NABWIRE AJIUNGA NA POWER DYNAMOS YA ZAMBIA

Kiungo wa Harambee Stars, Marvin Nabwire, amejiunga na klabu ya Power Dynamos ya Zambia kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Kenya Police FC.

Nabwire mwenye umri wa miaka 25 ameondoka Police baada ya kuisaidia klabu hiyo kutwaa Kombe la Mozzart Bet mwaka 2024 na baadaye kushinda taji lao la kwanza la Ligi Kuu ya FKF msimu wa 2024/2025.

Aidha, kiwango chake kizuri kilichomshuhudia akifunga mabao saba akiwa kiungo kilimrejesha katika kikosi cha Harambee Stars chini ya kocha Benni McCarthy, ambapo alichangia Kenya kufika hatua ya robo fainali ya mashindano ya CHAN.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *