BARCELONA YAMSAJILI KARIM ADEYEMI
Barcelona imemtambulisha rasmi mshambuliaji Karim Adeyemi baada ya kumsajili kutoka Borussia Dortmund kwa ada inayokadiriwa kufikia euro milioni 29, ikijumuisha nyongeza kulingana na masharti ya mkataba.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ametia saini mkataba wa miaka mitano utakaomuweka katika klabu hiyo hadi Juni 30, 2031, na kuwa usajili wa pili wa Barcelona baada ya kumnasa Anthony Gordon kutoka Newcastle United.
Adeyemi, anayejulikana kwa kasi yake na uwezo wa kucheza katikati au pembeni mwa safu ya ushambuliaji, anatarajiwa kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Barcelona kufuatia kuondoka kwa mshambuliaji mkongwe Robert Lewandowski.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































