#Local News

CHERARGEI ATAKA GACHAGUA AHOJIWE NA POLISI

Seneta wa Nandi, Samson Cherargei, amemtaka aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kurekodi taarifa kwa polisi kwa madai ya kuhujumu uchumi kupitia kauli zinazodaiwa kuwakatisha tamaa wawekezaji na watalii kuja nchini.

Akizungumza katika Bunge la Seneti, Cherargei pia ameitaka Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) kuchunguza kauli hizo na kuchukua hatua zinazostahili kwa mujibu wa sheria.

Seneta huyo amesema athari zozote kwa sekta ya utalii haziathiri Pwani pekee, bali pia maeneo mengine yanayotegemea utalii kama Nandi, Meru na Nanyuki, akisisitiza umuhimu wa kulinda uchumi wa taifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *